MJ THE ACTION

KARIBU MJ THE ACTION.COM

Alikiba Ajibu 'KIMTINDO' Mwaliko wa Diamond kwenye Wasafi Festival

Jana Novemba 5,  Diamond Platnumz alitangaza kuwa anatamani sana kumuona msanii mwenzake pia akiwa kama kaka yake kwenye muziki Alikiba awepo kwenye tamasha lake la Wasafi Festival .

Lakini baada ya Diamond kuongea hayo watu walianza kuzungumza mitandaoni na kuanza kusema Alikiba hawezi kukubali huku wengine wakisema Alikiba akubali tu, na hadi kufikia wengine kusema Alikiba atatoa jibu lake baya au la kizarau sana.

Sasa bila shaka taarifa hizo zimemfikia Alikiba ambapo muimbaji huyo ame-post picha ya mchekeshaji Mr. Bean ikiwa na maneno yanayosomeka; 'Thank you for listening, To my presentation', halafu chini ya post hiyo akaandika “Your welcome”

Mashabiki wengi wamechukulia kwamba hilo ndio jibu la Alikiba kwa Diamond kuhusu suala la yeye kushiriki Wasafi Festival ambayo itaanza November 24, 2018 mkoani Mtwara kisha kwenda Iringa na Morogoro. 
Alikiba Ajibu 'KIMTINDO' Mwaliko wa Diamond kwenye Wasafi Festival Alikiba Ajibu 'KIMTINDO' Mwaliko wa Diamond kwenye Wasafi Festival Reviewed by mjtheaction on November 06, 2018 Rating: 5

No comments:

Followers

Powered by Blogger.