MJ THE ACTION

KARIBU MJ THE ACTION.COM

BASATA Yaufungia Wimbo Mpya wa Diamond na Rayvanny- Mwanza (Nyegezi)


Baraza la Sanaa Tanzania (Basata) limetangaza kuufungia wimbo mpya wa mwanamuziki Rayvanny kwa maelezo kuwa unahamasisha masuala yasiyokubalika katika jamii.

Katibu Mtendaji wa Basata, Godfrey Mngereza amesema  kuwa wameufungia wimbo huo ambao amemshirikisha Diamond Platnumz na kupiga marufuku kuchezwa mahali popote.

Ameongeza kuwa wanawasiliana na mamlaka nyingine ili kuchukua hatua zaidi kwa kuwa tayari wimbo umeenea mitandaoni.

Kuhusu kupigwa katika tamasha lao la Wasafi linalotarajiwa kuanza kutimua vumbi Novemba 24 mwaka huu amesema nalo watalifungia iwapo watautumia.

Ameainisha kuwa maneno yaliyotumika katika wimbo huo yanahamasisha ngono kinyume na maumbile na matusi mengine yanayobomoa maadili.
BASATA Yaufungia Wimbo Mpya wa Diamond na Rayvanny- Mwanza (Nyegezi) BASATA Yaufungia Wimbo Mpya wa Diamond na Rayvanny- Mwanza (Nyegezi) Reviewed by mjtheaction on November 12, 2018 Rating: 5

No comments:

Followers

Powered by Blogger.